Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Chuo cha uuguzi Tarime kinatoa mafunzo bora ya afya kanda ya ziwa
Na Clonel Mwegendao
Katika kuhakikisha Vifo vya akina mama wajawazito na watoto vinapungua hapa nchini Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imeweka mikakati ya kuhakikisha tatizo la akina mama wanaojifungulia njiani na kupoteza maisha linatokomezwa kabisa na kubaki historia
Tatizo la vifo vya akina mama wajawazito bado ni changamoto kubwa hapa nchini kufuatia akina mama waliowengi hasa wa vijijini kutokuwa na Elimu juu ya kuhudhuria kliniki , Hali hiyo ikagusa Serikali kupitia Wizara ya Afya kuja na mpango kazi mbadala wa kutokomeza vifo hivyo kwa kuandaa wauguzi wenye sifa bora kwa kutoa elimu inayoruhusu mhitimu kuwa na uwezo wa kuhudumia jamii.
Akizungumza katika sherehe ya kukitambua chuo cha uuguzi Tarime kuwa ni chuo kinachotoa mafunzo bora kati ya vyuo bora vya afya kanda ya ziwa Ndemetria Vermand ambaye ni mkurugenzi msaidizi mafunzo ya wakunga wizara ya Afya amesema kuwa changamoto ya baadhi ya akina mama kujifungua wakiwa majumbani jambo ambalo linapelekea vifo kwa akina mama na watoto ,kwa kuliona hilo wizara husika inasimamia vizuri vyuo mbalimbali vya wakunga na wauuguzi hao ili kuepukana na kadhia hiyo
Hivyo jamii itarajie makubwa kukabiliana na vifo vya akina mama na watoto ambapo baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uuguzi na ukunga Tarime wakiwameweka bayana na kushukuru jitihada za walimu katika kuhakikisha wanapata ueledi katika sehemu hiyo na wanaondoa changamoto ya uhaba kwa elimu katika jamii suala ambalo husababisha tatizo hilo baadhi ya wakina mama na watoto kufariki wakati wa kujifugua .
Awali akieleza mafanikio ya chuo hicho Magabona Messe ambae ni mkuu wa chuo cha uuguzi na ukunga Tarime amesema kuwa umoja na mshikamano ndiyo siri ya mafanikio ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kujituma kuzingatia muda na kuongeza kuwa atakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha chuo hicho kinatoa wauguzi bora zaidi.
Hata hivyo Mkurugenzi mradi wa ukunga na watoto amekuwa akikatishwa tama na vyuo vya serikali kutofanya vizuri licha ya kuwa msimamizi wa vyuo hivyo na vyuo binafsi hivyo amefurahishwa na jitihada hzo zilizofanyika katika kuwezesha vyuo mbalimbali vya serikali vinafanya vizuri zaidi katika kutoa wataalamu wa afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment