Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Mbunge wa Babati Vijijni Jituson adhamini ligi kwenye Kata 25 jimboni kwake
Na John Walter-Babati,Manyara
Mbunge wa jimbo la Babati vijijini Jituson [CCM] amesema wamekuwa wakifanya vizuri katika soka lakini figisu figisu za viongozi wa chama cha Soka mkoa wa Manyara kimepelekea kukosekana kwa timu inayoshiriki ligi mbalimbali za kitaifa.
Amesema wilaya ya Babati vijijini zipo timu nyingi ambazo zinafanya vizuri akiitolea mfano Magugu Rangers na Krishna lakini zimekuwa zikifanyiwa hujuma ambazo zimekuwa zikiwafanya washindwe kuendelea mbele huku viongozi wa chama cha Soka Mkoa [MARFA] wakihusika katika kuzizoofisha jitihada za timu hizo.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi mipira na jezi kwa timu zilizofanya vizuri katika ligi ya mpira wa miguu iliyofanyika katika kata ya Ufana na kudhaminiwa na Mbunge huyo.
Amesema lengo la kudhamini Mashindano hayo yaliyoanzishwa na Chama cha mapinduzi wilayani humo ni kuendeleza vipaji ambavyo vipo katika eneo hilo.
Akizungumza na Muungwana Blog, Jituson amesema mashindano hayo yanayofanyika katika kata 25 za jimbo hilo yanaendelea ambako bingwa wa kila Kata anapatiwa vifaa vya michezo huku timu bora na yenye nidhamu pamoja na mchezaji bora wakipatiwa fedha taslimu.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Babati vijijini Filbert Mdaki, amesema michezo ni Miongoni mwa maelekezo ya ilani ya Ccm ,hivyo atahakikisha michezo hiyo inazidi kufanyika katika kila kijiji na kitongoji.
Amesema badala ya mpira wa miguu pekee yake sasa wanatanua zaidi wigo kwa kuongeza michezo mingine ya riadha,mpira wa miguu kwa wanawake,mpira wa mikono kwa wanawake na michezo mingine ili kuwaunganisha watu pamoja na kuifanya miili yao iwe na mazoezi ili kuepuka maradhi ya kisukari na presha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment