Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Wasichana wanaobalehe kusaidiwa kuepuka VVU


Serikali imezindua mradi wa miaka mitatu wa timiza malengo kwa wasichana balehe na wanawake vijana utakaosaidia kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Pia wakurugenzi wa Halmashauri 10 zinazotekeleza mradi huo wametakiwa kuhakikisha wanautekeleza kwa ufanisi mradi huo na wasiwe na urasimu na vikwazo katika utekelezaji wake.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika kijiji cha Chikola wilayani Bahi mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids), Dk Leonard Maboko alisema mradi huo ni wa majaribio katika mikoa mitatu na halmashauri 10 nchini.

Alisema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wasichana walio katika rika balehe walioko shuleni pamoja na wanawake vijana walioko mitaani ili waweze kuondokana na vishawishi vitakavyowasababishia kupata maambukzi ya virusi vya Ukimwi.

Dk Maboko alisema jumla ya walengwa 15,954 wasichana walio shuleni watanufaika kwa kupata fedha Sh 25,000 na taulo za kike kila mwezi kwa miaka mitatu.

Alisema pia wanawake vijana waliopo mitaani wapatao 14,295 watanufaika kwa kufundishwa stadi za maisha, ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambazo zitawasaidia kujikimu ili kuweza kuepukana na vishawishi vitakavyowatumbukiza kupata maambukizi ya Ukimwi.

"Wanafundishwa na kuandaa mpango wa biashara kwa kusaidiwa na maofisa ugavi na akiwasilisha huo mpango anapatiwa asilimia 60 ya fedha na baadaye anamaliziwa asilimia 40 iliyobaki, kiasi chenyewe cha fedha ni Sh 400,000 ambacho siyo haba katika mtaji wa biashara kwani kuna watu walianza na Sh 10,000 lakini leo wana mamilioni,"alisema.

Dk Maboko alisema kuwa mradi huo umekuja baada ya takwimu kuonesha kuwa asilimia 40 ya maambukizi mapya yako kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...