Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Mkuu wa Chuo ataka Wanafunzi wakihitimu Sekondari wapitie kwanza Veta
Na John Walter-Babati
Mkuu wa chuo cha Ufundi Stadi Veta Manyara Felix Olendukai ameishauri Serikali ya Tanzania na Wizara ya Elimu kubadilisha sera,kwamba mwanafunzi baada ya kumaliza sekondari kuwe na miaka miwili ya ufundi stadi ili kuweza kutimiza azma ya ya viwanda.
Ametoa ushauri huo kwa serikali baada ya kufanyika kwa makubaliano ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa tawi la Veta Mkoa wa Manyara ambalo linajengwa katika kijiji cha Ayasanda kata ya Ayasanda,lenye ukubwa wa Hekari kumi [10].
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza mafundi wengi ambao watakuwa na mchango mkubwa katika jamii.
Amesema wanaongeza tawi hilo ili kuongeza Udahili zaidi katika chuo hicho ambacho kwa sasa kina uwezo wa kudahili wanafunzi 460 pekee,idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na uhitaji.
Amesema kuwepo kwa tawi katika katika kijiji hicho cha Endanachan kata ya Ayasanda kutasaidia kukuza uchumi wa eneo hilo kwani biashara mbalimbali zitaendelea kufanyika ikiwemo ya vyakula na vifaa kwa ajili ya wanafunzi pamoja na kuongeza idadi ya watu wenye ujuzi katika kata hiyo.
Naye Mbunge wa Babati vijijini Jituson alieshuhudia Utiaji saini huo amesema fedha kwa ajili ya ujenzi wa tawi la chuo kutoka serikali kuu zimeshapatikana milioni 400 na kilichokuwa kinasubiriwa ni kijiji kukubali kutoa eneo hilo kwa Veta,kitendo ambacho kimekamilishwa leo.
Mbunge huyo amelishukuru shirika la Worl Vision kwa kujenga darasa,vyoo na nyumba ya walimu ili kuhakikisha wanapatikana watu wenye ujuzi kupitia mafunzo kutoka chuo cha Ufundi stadi [Veta].
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment