Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Jimbo la Kubenea, Mnyika 2020 lazima yarudi CCM - Mavunde


Naibu  Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amesema mwaka 2020 ni lazima majimbo mawili Ubungo na Kibamba yarudi  ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Jimbo la Ubungo likiwa nila Kubenea na Kibamba likiwa ni la Mnyika, yote haya yakiwa yanaongozwa na chama Upinzani (Chadema).

Akizungumza kwenye kampeni maalum inayoendeshwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema CCM itahakikisha Dar es salaam inakuwa ya kijani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

“Kama kuna uhitaji wa maji, barabara nzuri vyote vinafanyika sasa kuna haja gani ya kubakia upande wa pili wa upinzani ni lazima vijana kufanya kazi kuhakikisha majimbo yanarudi CCM na katika uchaguzi wa serikali za mitaa kata zote ziwe chini ya chama chetu.

“Jitahidini viongozi hii ni aibu anzeni na mitaa yote 91 kuhakikisha inarudi ndani ya CCM maana nikiangalia hapa hakuna kupita Mnyika wala Kubenea watapitia wapi?,’’amesema Mavunde.

Aidha Waziri huyo amesema makosa yalifanyika hapo awali yakuachia majimbo hayo kuchukuliwa na chama cha upinzani chini ya Mbunge, John Mnyika (Kibamba ) na Mbunge, Saed Kubenea (Ubungo), hayatafanyika tena kwa kuwa hakuna wanachokifanya zaidi ya kutekeleza ilani ya CCM.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...