Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Ramadhan Kabwili afikia sehemu nzuri ya mazungumzo na timu ya Sudan
Mlinda mlango wa timu ya Yanga SC, Ramadhan Kabwili ameeleza kuwa amefikia sehemu nzuri ya mazungumzo na uongozi wa timu ya Sudan hivyo anasubiri kwenda muda wowote kuanzia sasa.
Kabwili amesema kuwa mkataba wake na Yanga unakamilika Mei 30 hivyo bado anaendelea kuangalia ofa zilizopo mezani kabla ya kuondoka Yanga.
"Kweli kwa sasa ndani ya Yanga mkataba wangu unamalizika mwezi huu hivyo nina ofa ambazo zipo mkononi tunaendelea kufanya mazungumzo kabla ya kusaini ambapo ni timu moja ya Sudan ambayo tumefika sehemu nzuri.
"Mazungumzo yakikamilika kila kitu kitakuwa sawa, na nitaiweka wazi timu yenyewe, ila bado sijaikatia tamaa timu yangu ya Yanga kwa kuwa ni sehemu yangu ya kazi na wamenilea pia lazima iwe kipaumbele changu." amesema Kabwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment