Search This Blog

Saturday, May 25, 2019

Terminal 3 JNIA kukabidhiwa mapema


Jengo la Tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Terminal 3, Dar es Salaam litakabidhiwa mapema tofauti na ilivyoelezwa awali.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema, jengo hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka, litakabidhiwa Mei 29, ikiwa ni siku moja kabla tarehe ya awali iliyoahidiwa na mkandarasi.

Awali, mkandarasi aliahidi kukabidhi jengo hilo, Mei 30 kwa wamiliki, ambao ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuzinduliwa rasmi na Rais John Magufuli baadaye mwaka huu.

Tayari ujenzi wa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 99.5 na sasa vitu vikubwa vinavyofanyika ni kufunga vifaa mbalimbali, vikiwemo vile vya usalama, milango, viti na vile vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alisema kuwa tayari ujenzi umeshakamilika na watu wa TCRA, Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL), Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na wengineo wanaweka mifumo yao ya huduma ili kukamilisha ujenzi huo.

"Mtendaji Mkuu kwa sasa anahangaika na watoa huduma na wanaotakiwa ni wale wenye uwezo mkubwa na ambao hawafanyi kazi kwa mazoea na ni bora wakapatikana vijana wa kitanzania wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma katika jengo hilo bora kabisa na la kisasa,“ alisema Kamwelwe baada ya kukagua jengo hilo."

Alisema baada ya Mei 29, wataanza kufanya majaribio ya matumizi mbalimbali katika jengo hilo, ambalo halina tofauti kabisa na majengo ya viwanja vya Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea.

Pia Kamwelwe alisema baada ya kukamilika kwa jengo la terminal 3, ujenzi utahamia katika terminal 2, ambalo lenyewe litatumika kwa ajili ya abiria wa hapa nchini ambao wanatoka na kuwasili kutoka mikoa mbalimbali.




http://bit.ly/2X6RzoP

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...