Search This Blog

Saturday, May 25, 2019

RC aamua watumishi kusalimisha ATM kulinda maslahi


Serikali mkoani Shinyanya imeamua kuingilia kati kulinda masilahi ya watumishi wake ambao wamelazimika kusalimisha kadi zao za benki (ATM) kwa watu binafsi waliowakopesha akiwataka kuzikabidhi kwa wakuu wao.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack alisema kuwa ofisi yake imeagiza kufanyika kwa uhakiki wa mikopo binafsi ya watumishi wa umma, hasa wale wa halmashauri waliobainika kukopa hadi kufikia hatua ya kukosa mishahara mwisho wa mwezi ili kulinda masilahi ya pande zote mbili; wakopaji na wakopeshaji.

“Wote wanapaswa kuzingatia sheria, si nia ya Serikali kuwafanya waliowakopesha watumishi kupata hasara. La Hasha! Tunataka kulinda haki na masilahi ya pande zote kwa mujibu wa sheria, ndiyo maana mwezi huu tumeruhusu hata watumishi ambao hawajaitikia agizo la uhakiki wa ATM Cards zao, walipwe mishahara yao."

Wilaya ya Kishapu mkoani humo imeshachukua hatua na hivi karibuni ilitoa tangazo ikiwataka watumishi wake kusalimisha kadi hizo za benki. “Utafiti uliofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa umebaini kuwa wapo watumishi 269 waliosalimisha kadi zao za benki kwa waliowakopesha na wahusika (wakopeshaji) wameagizwa kurejesha kadi hizo kwa wamiliki,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era juzi.

Alisema siku ya mwisho ya kutekeleza amri hiyo ilikuwa juzi Mei 23, 2019.




http://bit.ly/2Ertlyv

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...