Search This Blog

Saturday, May 25, 2019

RC Mahenge awatahadharisha watendaji juu ya fedha za vitambulisho vya JPM


Na.Enock Magali,Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt,Binilith Mahenge amewatahadharisha watendaji wa kata pamoja na wale wote waliopewa jukumu la kuuza vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa ajili ya wajasiriamali kutothubutu kuzitumia fedha watakazo kuwa wamekusanya  kwa matumizi yao binafsi kwani zitawagharimu.

Dkt.Mahenge ameyasema hayo Wilayani Kondoa  katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua,kugawa,kutoa elimu na kuhamasisha wajasiriamali walio chini ya mtaji wa Shilingi Milioni nne kuwa na vitambulisho hivyo.

Akizungumza na watumishi mbalimbali wa Wilaya hiyo,amewataka kuwa waangalifu na fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya vitambulisho hivyo.

"Kuweni makini sana na vitambulisho hivyo,fedha mnayoipata iwasilisheni sehemu husika kwa uaminifu,hali ni mbaya mno msiziguse kabisa"Alisema

Aidha pia Dkt.Mahenge amegawa vitambulisho kwa wakuu wa Idara pamoja na watendaji wa kata zote za wilaya hiyo,huku akiwasisitiza kuongeza juhudi katia kuvisambaza kwa wafanyabiashara na kutomruhusu mtu yeyote kufanya biashara pasi kuwa na kitambulisho.

"Mtu ambaye hana kitambulisho haruhusiwi kufanya biashara,kila anaye fanya biashara ni lazima awe kwenye makundi mawili,kundi la kwanza ni lazima awe na leseni ya biashara na pili ni lazima awe na kitambulihso cha wajasiriamali na ni lazima akivae muda wote wa kazi,simamieni hili.Alisisitiza.

Na katika wakati huo huo amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kutii agizo na maelekezo ya Serikali juu ya katazo la matumizi ya mifuko ya Plastiki linaloanza kutekelezwa rasmi June Mosi mwaka huu.

http://bit.ly/2wlhpty

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...