Search This Blog
Saturday, May 25, 2019
DC Makete aagiza mwenyekiti wa kijiji akamatwe
Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Mh Veronica Kessy amemuagiza Afisa mtendaji wa Kata ya Kipagalo kushughulikia haraka madai ya wanawake wawili wa kata hiyo wanaodai kudhulumiwa malipo yao ya kusomba mchanga wakati wa ujenzi wa ghala la Matunda katika kijiji cha Madihani.
Mkuu wa wilaya ametoa agizo la kukamatwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Madihani Abinel Mbilinyi na mwananchi aliyetambulika kwa jina moja la Thomasi baada ya kuruhusu wananchi kutoa maoni yao kuhusu ghala hilo kabla halijakabidhiwa rasmi kwa serikali, ambapo mwanamama Jenifa Mbwilo amejitokeza na kudai kuwa hajalipwa na mkandarasi shilingi 150,000/- yeye pamoja na mwenzake kutokana na kufanya kazi ya kusomba mchanga.
“Mtendaji wa kata hawa wa mama wapate haki yao, kamata mwenyekiti wa kijiji,Thomas watoe hiyo fedha hawa wamama wapate haki yao na unipe ripoti, jumatatu ijao nipewe mrejesho kwamba wamelipwa pesa yao tumeelewana, tunataka mkandarasi aondoke akabidhi kazi yake bila madoa”alisema DC.
Awali akina mama hao akiwemo Jenipher mbwilo mbele ya mkuu wa wilaya amesema kuwa walikuwa wakisomba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa ghala hilo lakini mpaka sasa hawajamaliziwa madai yao.
“Tulikuwa tunasomba mchanga kwa hiyo hatujamaliziwa madai yetu tulikuwa wawili na mwenzangu mkandarasi bado hajatulipa”alisema Jenipher.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Abinel Mbilinyi amesema kuwa taarifa hizo anazo lakini inasemekana walidhulumiana kwani pesa yao ililipwa.
“swala hili ninalijua lakini hawa walikuwa na kiongozi wao na pesa hizo zililipwa sasa inasemekama walidhulumiana kwa hiyo inawezekana kiongozi wao ndio aliyewadhulumu,ila hili tatizo tulishalimaliza kwasababu tulikaa kwa maana kiongozi wao hawa atawalipa fedha”.
Ghala ya kuhifadhia matunda lililokuwa likijengwa katika kijiji cha Madihani wilayani Makete limekabidhiwa kwa serikali likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.1 hadi kukamilika kwake.
http://bit.ly/2QmtIzb
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment