Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
RC Gambo awachana watoa huduma wa NHIF
Serikali imewataka Watoa Huduma waliosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuachana na udanganyifu katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake kwa kuwa jambo hilo ni kurudisha nyuma maendeleo ya Mfuko ambao ni nguzo kubwa katika utoaji wa huduma za matibabu.
Akifungua kikao cha Wadau wa NHIF, Mkoa wa Arusha. Mrisho Gambo amesema kuwa udanganyifu katika huduma ni adui mkubwa wa uimarishaji wa chombo hicho ambacho kwa sasa kinahudumia wananchi wengi na wanaohitaji huduma ambazo gharama zake ni kubwa.
“Niwaombe sana wadau wote hususani wanachama wa Mfuko, ni vyema kila mmoja kwenye nafasi yake akawa mlinzi wa huduma anazopata ili Mfuko huu uwe imara zaidi na uendelee kuhudumia wananchi, mimi binafsi nikiri tu kwamba bila ya kuwa na kadi ya NHIF nisingeweza kumudu gharama za matibabu, nimemuuguza Mama yangu na alihitaji matibabu yenye gharama kubwa lakini kwa kuwa na kadi ya NHIF ilinisaidia kwa kiasi kikubwa sana, hivyo ili Mfuko huu uendelee kuwepo ni lazima sote kwa pamoja tuulinde,” alisema Bw. Gambo.
Kwa upande wa watoa huduma aliwataka kuwa wakweli na kuwa wazalendo katika vipimo na dawa wanazowaandikia wanachama ili Mfuko uweze kulipa gharama halisi na sio kulipa fedha ambazo huduma zake hazikuwa sahihi.
“Lengo la Serikali inayoongozwa na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona kila wilaya nchini inakuwa na Hospitali na kata inakuwa na kituo cha Afya na Kijiji kinakuwa na Zahanati ili upatikanaji wa huduma za matibabu uwe rahisi na bora zaidi na kwa kutumia mfumo wa Bima ya Afya wananchi watakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote,” alisema Bw. Gambo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda amesema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha mpaka ifikapo mwakani zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania iwe inahudumiwa na Mfuko na kwa upande wa huduma, Mfuko umejipanga kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma katika maeneo yao na kwa ubora unaotakiwa.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa NHIF, Bw.Bernad Konga amebainisha kuwepo kwa mifumo mizuri ya udhibiti wa udanganyifu ambayo mpaka sasa imeleta matokeo makubwa kwa kuokoa zaidi ya shilingi Bilioni 4 ambazo zingeweza kulipwa kutokana na vitendo vya udanganyifu vya baadhi ya watoa huduma.
http://bit.ly/2EvtSPR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment