Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
RC aliyetenguliwa na Rais Magufuli atoa neno kwa Watanzania
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa mpya wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homela ambaye aliteuliwa na Rais Dkt, John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Akizungumza katika makabidhiano hayo amesema amekitumikia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa vijana (UVCCM) kwa Muda mrefu na vipaji, uzoefu alionao atandelea kuwa Kada mwaminifu wa mstari wa Mbele wa Chama cha Mapinduzi
Amos Makalla amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka minne iliyopita akiitumikia mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Katavi katika uongozi Serikali ya Awamu ya Nne na ya Tano
Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki mwananchi na mwana (CCM) tu huko Mvomero lakini Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na baadaye Katavi.
Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela.
http://bit.ly/2X4Ne5F
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment