Search This Blog

Thursday, May 23, 2019

Airport sio uchochoro wa kupitisha magendo - IGP Sirro


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP,  Simon Sirro amesema kuwa, maeneo ya viwanja vya ndege hususani kiwanja cha ndege Dar es salaam kamwe hakitakuwa uchochoro wa kupitisha na kusafirisha magendo, biashara ya binadamu, nyara za serikali pamoja na dawa za kulevya.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal III kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho ambacho hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

Aidha, IGP Sirro, amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo kiwanjani hapo na kwamba hakuna mtu atakaye jaribu kuutumia uwanja mpya wa ndege terminal III kwa vitendo vya kuhujumu uchumi wa taifa letu.




http://bit.ly/2X4NfGL

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...