Search This Blog
Sunday, May 26, 2019
Nina furaha ya kuweza kuongeza miaka miwili - Tshishimbi
Mchezaji wa Yanga SC, Papy Tshishimbi ameeleza kuwa ameongeza mkataba Yanga sasa mambo yatakuwa biyee na ataipa ubingwa msimu ujao.
Tshishimbi ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu bara kufuatia mkataba wa kwanza kumalizika alijiunga na timu hiyo akitokea Mbabane Swallows ya Eswatini.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Tshishimbi alisema kuwa ana furaha ya kuongeza mkataba wa miaka miwili katika timu hiyo kwani malengo yake ni kutaka kuipa ubingwa wa msimu ujao.
"Nina furaha ya kuweza kuongeza miaka miwili katika timu yangu, naamini Yanga ni timu bora tofauti na nilipokuwa nacheza awali, Miaka miwili katika mkataba wangu nadhani nitafanya kilicho bora ili tushinde makombe nikiwa katika hii timu kubwa na hilo ndiyo lengo la kubaki kwangu,” alisema Tshishimbi.
http://bit.ly/2W11FLw
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...

No comments:
Post a Comment