Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Mbwana Samatta atoa ahadi kwa Watanzania kuhusu AFCON


Mshambuliaji wa klabu ya Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amewaahidi Watanzania kuwa atajitahidi kwa uwezo wake kuongoza vyema Taifa Stars katika michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON mwezi ujao nchini Misri.

Samatta ameyasema hayo baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitokea nchini Ubelgiji katika klabu yake ya Genk.

"Baada ya muda mrefu sana tumepata nafasi hii ya kwenda kushiriki, ukweli ni kwamba ni uzoefu mkubwa sana tunakwenda kuupata kutokana na uchanga wa timu yetu ya taifa kwa sababu hatujakuwepo kwenye mashindano kwa muda mrefu", amesema Samatta.

"Mpira siku zote una matokeo ya kushangaza, inawezekana tukawa wachanga kwa sababu ya muda mrefu kutoshiriki lakini tukafanya vizuri. Mimi kama kampteni naichukua timu yangu, tunaenda kushiriki na kupambana kuhakikisha tunapata kitu", ameongeza.

Pia Samatta amezungumzia juu ya ndoto yake ya kucheza soka nchini Uingereza, ambapo amesema, "huwezi jua kinachokuja mbele lakini mimi siku zote toka nikiwa mtoto tulikuwa tunaenda kwenye mabanda ya kuonesha mpira na nilikuwa mmoja wapo ambaye nilikuwa napenda kuangalia EPL, ni kitu ambacho kinanivutia sana. Napenda kucheza ligi ya Uingereza lakini huwezi jua itakuwaje".




http://bit.ly/2HUqKOt

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...