Search This Blog

Thursday, May 23, 2019

Nimeota ndoto mbaya kwa viongozi - Dkt. Bashiru


Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally amesema kuna jambo baya litawapata iwapo hawasimamia vyema maendeleo ya sekta ya kilimo.

Dk Bashiru amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa , ameota ndoto mbaya iwapo viongozi wa wizara hiyo watashindwa kusimamia vyema vyombo vitatu vya maendeleo ya kilimo vilivyopo chini yao.

“Kila zao limewekewa bodi. Kuna Bodi ya Miwa, Bodi ya Sukari, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Pamba, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Pareto, Bodi ya Chai, Bodi ya Korosho bodi, Bodi ya Kusimamia Mazao ya Kimkakati na hii Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko. Tunataka utitiri huu wa bodi za kinyonyaji uondoke kwa kuziunganisha. Hilo wazo lipo wizarani linachakatwa; mchakato huo ukamilike tuwe na vyombo viwili vya mazao. Bodi ya mazao mchanganyiko na Bodi ya Mazao ya Kimkakati,” alisema Dk Bashiru katika ziara yake ya kukagua miradi na maendeleo ya chama hicho tawala mkoani Mwanza.

Akivitaja vyombo hivyo kuwa ni bodi za mazao, tume ya ushirika na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alizosema hazijafanya vya kutosha kusaidia sekta ya kilimo aliyosema ndivyo imebeba ufanisi kwenye ajenda ya Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025 kupitia mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya sekta ya kilimo.




http://bit.ly/2EqtwKc

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...