Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
Kesi ya mfanyabiashara aliyejeruhi yapigwa Kalenda
Kesi ya kujeruhi watu wawili kwa kuwakata masikio inayomkabili mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha, Anselim Minja, imeahirishwa hadi Juni 21 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arumeru, Amalia Mushi ,Minja anadaiwa kuwakata masikio ya kushoto Samwel Sembeke na Aloyce Petro, ambao kwa sasa wanadaiwa kupata ulemavu wa kudumu.
Wakili wa Jamhuri, Ahmed Khatibu aliieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo upo katika hatua za mwisho na kuiomba Mahakama iiahirishe.
Hakimu Amalia aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 21 mwaka huu ambapo Minja alikuwa akitetewa na Wakili Innocent Mwanga, ambaye hakuwa na pingamizi na maelezo hayo ya Wakili wa Jamhuri.
Minja ambaye anamiliki biashara mbalimbali jijini hapa ikiwemo pamoja na shule ya kujifunzia udereva wa magari(Modern Driving School), kwa mara ya kwanza alifikishwa kizimbani Machi 28 mwaka huu.
Awali mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Obadia Bwegego, akimsomea mashitaka hayo Wakili Mwandamizi wa Serikali, Martenus Marandu, alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo Julai 21 mwaka 2017, katika eneo la Njiro jijini hapa.
Alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo huku akijua ni kinyume cha sheria, ambapo alidai kuwasababishia watu hao ulemavu wa kudumu baada ya kitendo hicho cha kikatili.
http://bit.ly/2X71HhG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment