Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Mataifa 21 yashiriki uchaguzi wa Bunge la Ulaya


Vituo vya kupigia kura vya nchi wanachama 21 wa Umoja wa Ulaya vitafunguliwa leo Jumapili, kwa uchaguzi wa bunge la Ulaya ikiwa ni pamoja na mataifa makubwa ya umoja huo ambayo ni Ujerumani, Ufaransa, Italia, Uhispani na Poland.

Mataifa hayo matano pekee yanatoa takriban nusu ya wabunge wa Bunge la Ulaya ambao ni 348 kati ya jumla ya wabunge 751.

Upigaji kura wa bunge pekee la kimataifa duniani ulianza Alhamis nchini Uholanzi na Uingereza, Ireland na Jamhuri ya Czech zilipiga kura hiyo Ijumaa iliyopita na Latvia, Malta pamoja na Slovakia zilipiga kura jana Jumamosi.

Jumla ya wananchi milioni 420 wana haki ya kupiga kura, Watafiti wanatarajia idadi ya wananchi watakaojitokeza kupiga kura itaongezeka kidogo ikilinganishwa na asilimia 43 tu ya mwaka 2014.

http://bit.ly/2WkNr7P

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...