Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Mbunge aumizwa na Utapiamlo, atoa somo kwa Wananchi


Na John Walter-Babati.

Mbunge wa Babati Vijijini Jituson [CCM] ambaye pia ni mtendaji katika kamati ya lishe, amewataka  wakina mama wajawazito kuzingatia kula lishe bora  kwa siku elfu moja za mwanzo kuanzia mimba inapotungwa hadi kuzaliwa ili kumuepusha mtoto na tatizo la Utapiamlo.

Mbunge Jitu amesisitiza hilo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mandi, Maganjwa na Sabilo kata ya Dabili alipowatembelea katika ziara yake inayoendelea katika jimbo hilo.

Amesema cha kushangaza mikoa yenye hali mbaya katika suala la Lishe na udumavu ni mikoa mitano ya Nyanda za juu kusini ambayo inazalisha chakula kwa wingi ikifuatiwa na mkoa wa Manyara kwa upande wa kanda ya kaskazini wenye asilimia 36 ya Lishe duni na utapiamlo wakati mikoa ya Dar es salaam na Zanzibar ambayo haizalishi ina kiwango kidogo cha asilimia 1.

“Mtoto ambaye amedumaa na kuwa na utapiamlo na ubongo wake unaanza kuathirika na ukishaathirika hakuna namna ya kurekebisha ni ya kudumu kwa hiyo ni muhimu tujikumbushe”.

“Wakina mama wanafanya vizuri kwa sababu wakienda Kliniki wanakumbushwa lakini wakina baba endeleeni kuwakumbusha wake zenu”alisisitiza Mbunge huyo.

Kadhalika alisema uandaaji mzuri wa lishe kwa watoto huchangia kwa kiwango kikubwa kuepusha na magonjwa na kumjengea  uwezo wa kufanya vizuri darasani.

Amewaasa wakina baba kuhakikisha wanamhudumia mama vizuri ili aweze kutengeneza maziwa ya mtoto ambayo ndiyo muhimu kwa mtoto tangu anapozaliwa hadi mwaka mmoja na na  nusu.

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Jitu amewakumbusha wananchi kuweka akiba ya chakula kwani mwakani kuna hatari ya kuwa na njaa kutokana na mvua kuchelewa kuanza. 




http://bit.ly/2M9tP2m

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...