Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Kutunisha misuli yaweza kuathiri uwezo wa kuzaa



Wanasayansi wamegundua kuwa baadhi ya wanaume hupunguza uwezo wao wa kupata watoto kutokana na jitihada zao za kutengeneza miili ya kuvutia . Mazoezi ya kutunisha misuli au kutumia dawa za kuzuia kupata upara zinaweza kuharibu mfumo wa uzazi. Athari hiyo imetajwa mara baada ya wanasayansi kufafanua madhara hayo.

Wataalamu wanasema kwamba mwanaume anayetumia dawa au anayefanya mazoezi ya kutunisha misuli anaweza kuwa anapata maumivu ya kichwa wakati wa tendo la ndoa na mbegu zake kushindwa kuwa na uwezo wa kuzalisha.

"Nimegundua kuwa baadhi ya wanaume ambao wanakuja kwa ajili ya vipimo miili yao huwa ni mikubwa," alisema Dkt James Mossman, kutoka chuo cha Brown kilichopo Marekani. Daktari huyo ameiambia BBC kuwa : "Wanaume wanajaribu kutaka kuwa na muonekano mkubwa, huku wanajisababishia madhara ya afya ya uzazi"

"Licha ya kuwa wanajitengeneza wenyewe maumbile yasiyokuwa na uhalisia, lakini wanashindwa kuelewa kuwa wanajiondolea uwezo wao wa kuwa na mbegu za kuzalisha."

Miongoni mwa madhara yanayowapata ni homoni zao kushindwa kufanya tendo la kujamiiana kiufasaha kutokana na mazoea yao ya kutengeneza muonekano wa miili yao kuwa chanzo. Profesa Allan Pacey kutoka chuo chaSheffield ameongeza : " Inashangaza kuona wanaume wanaenda kwenye mazoezi ili kuwa na muonekano mzuri, na mara nyingi lengo ni kuwavutia wanawake na bila kuelewa kuwa wanapunguza uwezo wao wa kuzaa."

Hata hivyo watafiti wanasema kwamba dhana inayofanana na hiyo ya wanaume kutumia dawa ili kutengeneza maumbile yao ina madhara yanayofanana.





No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...