
Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd Maganga amezungumzia suala la mchezaji wao Tafadzwa Kutinyu ambaye amenaswa na Horoya Athletic Club ya Guinea akiungana na Heritier Makambo wa Yanga.
"Kutinyu mkataba wake na Azam unakwisha mwisho wa mwezi huu, chama cha soka cha Zimbabwe kilituandikia barua kumhitaji Kutinyu kwa ajili ya mashindano ya COSAFA kwa hiyo alishaondoka kwenda Zimbabwe."
"Lakini alishaomba mkataba ukiisha atakuwa na mipango mingine ya utaratibu wake wa maisha ya soka na ni mchezaji huru kwa hiyo ananafasi ya kuchagua pakwenda."
Afisa habari wa Azam alimalizia kwa kusema kuwa Kutinyu hatokuwepo tena Azam na amekuwa mchezaji wa kwanza anawapa nafasi ya kutafuta mchezaji mwingine."
No comments:
Post a Comment