Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Ajeruhi watu 17 kwa kuwachoma na visu
Watu wawili akiwemo mtoto mmoja wanahofiwa kupoteza maisha huku wengine 17 wakijeruhiwa katika shambulio kubwa la uchomaji visu katika mji wa Kawasaki nchini Japan.
Maafisa wa zimamoto wanasema, tukio hilo limetokea majira ya asubuhi hii leo, ambapo mwanaume mmoja aliwashambulia watu kwa kuwachoma visu.
Kwa mujibu wa mashuhuda mshambuliaji aliwalenga wanafunzi katika kituo cha basi. Polisi wanasema mshukiwa tayari amekamatwa, na ripoti za shirika la habari la Japam NHK, ni kwamba mshambuliaji huyo pia alijichoma visu na alikuwa na majereha makubwa.
Japan ni nchi iliyo na viwango vya chini vya uhalifu na mashambulizi makubwa yamekuwa nadra sana. Mwaka 2018 mwanaume mmoja alikamatwa baada ya kumshambulia kwa kisu na kumuua mtu mmoja huku wengine wawili wakijeruhiwa ndani ya treni. Tukio hilo lilichochea hatua za usalama kuimarishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment