Search This Blog

Monday, May 27, 2019

Kinyang'anyiro cha kuwania Uwaziri Mkuu wa Uingereza chapamba moto


Kinyang'anyiro cha kuwania wadhifa wa waziri mkuu wa Uingereza kimepamba moto, baada ya hivi leo Waziri wa Mazingira Michael Gove kujiunga na orodha ndefu ya wanasiasa wanaotaka kumrithi Theresa May aliyejiuzulu Ijumaa iliyopita.

Wanasiasa waliokwishatangaza kuwania wadhifa huo wana mitazamo inayotofautiana juu ya namna Uingereza itakavyojitoa Umoja wa Ulaya.Kujiuzulu kwa Bibi May kumeongeza uwezekano wa Uingereza kuondoka kutoka Umoja huo bila ya mkataba ifikapo Oktoba 31, ambayo ni tarehe ya mwisho iliyowekwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Miongoni mwa wagombea wanane wanaotaka kumrithi May wamesema watajaribu kutafuta mabadiliko kwenye mkataba uliofikiwa na Umoja wa Ulaya mwaka uliopita lakini wanajiweka tayari kwa uwezekano wa kuiondoa Uingereza bila mkataba wowote iwapo juhudi zao zitakataliwa.

 Umoja wa Ulaya umesema hautojadiliana upya vipengele vya mkataba uliofikiwa na waziri mkuu anayeondoka madarakani.

http://bit.ly/2VS7hD5

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...