Search This Blog

Monday, May 27, 2019

Chelsea yapata pigo kuelekea mchezo wa fainali

Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante anaweza kuukosa mchezo wa fainali ya Europa League kutokana na kupata majeruhi kwenye mazoezi jana.

Kante anategemewa kutazamwa kwa ukaribu maendeleo ya afya yake kabla ya fainali hiyo itakayochezwa uwanja wa  Baku dhidi ya Arsenal Mei 29.

Maurizio Sarri  Meneja wa Chelsea amesema kuwa bado anamtazama kijana wake kwa ukaribu kabla ya kufanya maamuzi ya kumtafutia mbadala wake kwenye mchezo wake huo muhimu.

Wachezaji wengi wa Chelsea ni majeruhi wanasumbuliwa na mifupa, ikiwa ni pamoja na Callum Hudson-Odoi, Ruben Loftus-Cheek na Antonio Rudiger wote wapo kwenye maumivu makali.

http://bit.ly/30Kzq2E

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...