Search This Blog
Monday, May 27, 2019
Rais wa zamani wa Botswana ahamia chama cha upinzani
Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, ametangaza kukihama chama tawala baada ya kuongezeka tofauti za kisera kati yake na rais aliye madarakani. Uamuzi huu unatajwa kutishia kukigawa chama tawala kilichoiongoza Botswana tangu ilipopata uhuru mwaka 1966.
Akiwahutubia wafuasi kadhaa katika mji wa kaskazini mashariki wa Serowe jana Jumamosi, Khama alisema atauunga mkono muungano wa upinzani, UDC, wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba. Mwanasiasa huyo amesema atafanya kazi na upinzani kuhahakisha chama tawala, BDP, kinaangushwa kwenye uchaguzi huo.
Khama aliyesalia kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama tawala cha BDP alikabidhi madaraka kwa aliyekuwa makamu wake, Mokgweetsi Masisi, mwaka uliopita baada ya kuingoza Botswana kwa muongo mmoja.
Lakini tangu alipochukua madaraka, Masisi amekuwa akitofautiana mara kadhaa na kiongozi huyo wa zamani, ikiwemo uamuzi wake wa kuondoa marufuku ya uwindaji wanyama katika mbuga nchini humo iliyowekwa na serikali ya Khama mwaka 2014.
http://bit.ly/30DR1sO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment