Search This Blog

Thursday, May 23, 2019

Amuua mtoto wake baada ya kujisaidia ndani ya nyumba


Mtoto wa miaka 10 amefariki nchini Kenya baada ya kupigwa na Baba yake. Inaelezwa kuwa mtoto huyo aliugua tumbo ghafla, hali iliyosababisha atapike na kujisaidia ndani ya nyumba.

Imebainika kuwa Mtoto huyo alikula chakula kilichomletea shida kwenye tumbo lake na wakati huo hakukuwa na Mtu wa kumsaida nyumbani.

Baada ya Baba yake kurudi na kukutana na hali hiyo alianza kumpiga bila ya kujali ugonjwa wake lakini baada ya kuona hali ya mtoto inabadilika aliamua kumkimbiza Hospitali.

Mtoto huyo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitalini hapo. Kesi ya Mwanaume huyo itasikilizwa Juni 3, 2019.

http://bit.ly/2HR3Abz

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...