Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
Airpot siyo kichaka cha kupitisha magendo - IGP Sirro
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, maeneo ya viwanja vya ndege ususan kiwanja cha ndege Dar es Salaam kamwe hakitakuwa uchochoro wa kupitisha na kusafirisha magendo, biashara ya binadamu, nyara za serikali pamoja na dawa za kulevya.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) terminal III kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho ambacho hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Aidha, IGP Sirro, amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo kiwanjani hapo na kwamba hakuna mtu atakaye jaribu kuutumia uwanja mpya wa ndege terminal III kwa vitendo vya kuhujumu uchumi wa taifa letu.
Naye Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Paulo Rwegasha, amesema kuwa, wameendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti vitendo vyote vya uhalifu vinavyotokea kiwanjani hapo na kwamba hadi sasa kutokana na ushirikiano uliopo wamefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa uhalifu.
Wakati huo huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amefanya ziara ya ukaguzi katika kikosi cha kutuliza ghasia FFU Ukonga Dar es salaam na kuzungumza na maofisa na askari wa vyeo mbalimbali ambapo katika ziara yake amewapandisha vyeo askari wawili kuwa sargent
http://bit.ly/2wovruJ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment