
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amebuni "jopo maalum" kusuluhisha kile alichotaja kuwa mzozo "hatari zaidi" wa kisiasa nchini humo tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2019, shirika la habari la serikali la Suna limeripoti.
Bw. Hamdok ametangaza jopo, ambalo linajumuisha wanachama kutoka makundi pinzani ya kisiasa, wakati wa mkutano wa "dharura" wa baraza la mawaziri siku ya Jumatatu mjini Khartoum.
Ametoa wito wa uvumilivu na kujadiliana kwa amani ili kukomesha wiki kadhaa za taharuki ya kisiasa ambayo imetishia kuvuruga utawala wa awamu ya mpito kuelekea uaongozi wa kidemokrasi.
Kauli yake inajiri baada ya polisi kuwatawanya waandamano wanaounga mkono utawala wa kijeshi ambao wanashinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpito.
Maandamano yalianza Oktoba 16 mbele ya Ikulu ya rais kutaka jeshi lichukue madaraka.
No comments:
Post a Comment