Search This Blog

Tuesday, October 19, 2021

Urusi imesimamisha ushirikiano wake na NATO


Urusi imesimamisha ushirikiano wake wa Jumuiya ya Kujihami NATO na kuamuru kufungwa ofisi ya muungano huo ya mjini Moscow katika kile kinachoelezwa kuwa ni hatua ya kulipiza kisasi baada ya NATO kuwafurusha wanadiplomasia wa Urusi.
 
 Mapema mwezi huu, NATO iliwaondolea idhini wanadiplomasia wanane wa Urusi katika makamo makuu ya jumuiya hiyo mjini Brussels, kwa kusema ina amini wanafanya kazi kwa siri kama maafisi wa kijasusi wa Urusi. 
 
Lakini pia umoja huo umepunguza idadi ya maafisa wa Urusi katika makao makuu yake kutoka watu 20 hadi 10.Urusi imeyatupilia mbali madai hayo kwa kusema hayana msingi wowote. 
 
Na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov jana Jumatatu akatangaza kusitisha shughuli za Urusi katika jumuiya ya NATO na pamoja na ofisi ya mawasiliano ya mjini Moscow.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...