Search This Blog

Monday, October 11, 2021

Watu zaidi ya milioni 900 wana ugonjwa wa akili duniani


Kila tarehe 10 october watu wanaadhimisha  siku ya Afya ya akili duniani,kwa Tanzania mahadhimisho hayo yamefanyika "TGNP" na taasisi binafsi ya @marcusmwemezifoundation16 na kauli mbiu inasema "Afya ya Akili duniani isiyo na usawa" Sophia Samson Sanga Muuguzi katika idara ya afya na magonjwa ya akili katika hospitali ya taifa muhimbili amesema watu zaidi ya milioni 900 wana ugonjwa wa akili Duniani na kila baada ya ya sekunde 60 kuna mtu anajiua.

Aidha kwa upande mwingine amesema sababu inayosababisha watu wengi kuwa na ugonjwa wa akili ni pamoja na kufeli darasani, kutumia Madawa ya kulevya, Mapenzi  na kutumia vilevi kupita kiasi "watu wengi hawafahamu afya ya akili ni nini na wagonjwa wengi wenye matatizo ya akili hawawezi kujielezea mpaka inapelekea kufanya maamuzi magumu ya kujiua" sophia Sanga muuguzi hospital ya Taifa muhimbili.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...