
Mwanamuziki maarufu Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Delcato Idengo, amekamatwa na polisi kwa baada ya kushutumiwa kuhamasisha ghasia dhidi ya vikosi vya usalama katika eneo la kaskazini mashabiki.
Mwanamuziki huyo alikamatwa Jumapili huko kaskazini mashariki katika mji wa Butembo.
Mashabiki wake walifanya maandamano wakitaka aachiwe huru.
Polisi wa Idengo wamesema watamshtaki kwa kosa la kuhamasisha vurugu dhidi ya polisi na jeshi. Hajapelekwa mahakamani bado.
Miziki ya Mwanamuziki huyo mara nyingi huwa inakosoa serikali haswa kwa kushindwa kurejesha amani mashariki mwa Kongo.
Awali aliwashutumu polisi kwa kutofanya lolote kuzuia ghasia.
No comments:
Post a Comment