Search This Blog
Wednesday, October 6, 2021
Wafugaji na wajasiliamali wamemuomba Serikali kutenga maeneo rasmi ya machinjio ya kuku
Na Maridhia Ngemela.
Wafugaji wa kuku,wavuvi na wajasiliamali wameiomba Serikali kuwatengea maeneo maalum ya uchinjaji kuku na maeneo maalum ya kuuzia nyama hizo ili kuendana na utandawazi uliopo ,kujiepusha na maradhi.
Wameyasema hayo leo hii mkoani Mwanza ukumbi wa Nyanza walipokuwa katika mafunzo ya wafugaji na wavuvi kwa lengo la kuendelea nikumbusha na kupeana mikakati itakayoleta Tija katika shughuli zao za kuwaingizia kipato.
Rosemary mwakisalu ni miongoni mwa wajasiliamali kutoka Wilaya ya Ilemela walioiomba Serikali kuwatengea maeneo maalum ya uchinjaji wa kuku na bucha za kuuzia nyama hizo kutokana na gharama kubwa ya ufugaji wanayoipata na inapofikia muda wa uuzaji wanauzwa kwa bei rahisi na kupelekea kutothaminiwa kwa kitoweo hicho ambacho ni pendwa kwa Watanzani.
"Amesema Mimi nadhani kwa upande wa kuku Serikali itutengenezee bucha na mazingira kama walivyowatengenezea wauzaji wa nyama ya ng'ombe,kondoo ili sisi wafugaji unapokuwa na kuku wako unajua nitaenda sehemu Fulani kwaajili ya kuuza kukuzangu lakini hii kiholela holela unajikuta unatumia gharama kubwa katika ufugaji ila kwenye uuzaji unauza kwa bei ya kuumizana amesema Rosemary.
Mwenyekiti wa Umoja wa wajasiliamali wa kuku amesema wanaumoja hao wanauhitaji Umoja na Serikali wanauhitaji kuwa na bucha za uuzaji wa kuku ili kuondoa usumbufu wanaopata wafugaji katika soko la uuzaji wa kuku na Serikali iingilie Kati wauzaji wa mayai wanaotoka Nchi za nje ilikuwapa nafasi wafugaji wa Tanzania waweze kufurahia kazi zao za ufugaji.
Naye Dk.msomi Antipachius Anthony kutoka bodi ya nyama Tanzania ofisi ya Kanda ya ziwa amesema uchinjaji wa nyama holela upo Mkoani Mwanza na kwa sasa wanatembea Wilaya kwa wilaya kuendelea kutoa elimu juu ya kuacha uchinjaji huo ambao hauna tija kwa mlaji na mfugani.
"Huo ubora wa nyama unaouona buchani inategemea na mfugo unalishwaje,unafugwaje na uchinjaji huo wa holela upo katika Mkoa huu kwahiyo sisi kama bodi ya nyama tunaendelea kushirikiana vizuri kwa kuwapatia elimu ya uchinjaji ,uuzaji unakuta kwenye bucha unakuta nyama inaninginizwa nje nzi zinapita,mondo nyeusi kuna migogo humo na ukizingatia katika kipindi cha mvua maradhi ni mengi kwa hiyo tutaendelea kushirikiana na wauzaji,wafugaji kwa kuwapatia elimu ya uchinjaji wenye tija na tunashukru maeneo tunayopitia wanaelewa na wanabadirika kabisa kwahiyo tunataka mwisho wa mwaka huu uchinjaji holela na uuzaji wa nyama uwe umekwisha lengo letu ni hilo amesema Anthony.
Kwa upande wake mgeni rasmi akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza katibu tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji Emil Kasagara alipokuwa akifungua mafunzo hayo amesema katika uboreshaji wa koosafu za mifugo mkoa kwa kushirikiana na Shirika la Land I'm Lake unaendelea na uboreshaji wa mifugo kwanjia ya uhimilishaji na kutumia madume bora na wataendelea kuweka mikakati bora ya kupambana na magonjwa ya mifugo kwani wizara ya mifugo na uvuvi imeendelea kutoa dawa za kuogesha mifugo katika Mkoa huo.
" Mkoa una jumla ya minada 12ya swali iliyopo chini ya usimamizi wa Halmashauri na mnada 1wa upili upo chini ya wizara ya mifugo na uvuvi uliopo Wilaya ya misungwi kwahiyo najaribu kuelezea hivyo ili mjue kuwa Serikali iko kazini jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili hata nyie wafugaji wa kuku msijione kama mmetengwa changamoto mlizozieleza nitazipeleka mkoa utasimamia utaratibu mzuri kabisa kwahiyo fanyeni kazii kwa amani amesema Kasanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment