Search This Blog

Wednesday, October 20, 2021

Waendesha mashtaka wakata rufaa juu ya hukumu dhidi ya shujaa wa Hotel Rwanda


Waendesha mashtaka wamewasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa korti juu ya Paul Rusesabagina, mtu aliyeonyeshwa kama shujaa katika sinema ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Rusesabagina, 67, alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwezi uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuunga mkono kundi la waasi lililohusika na mashambulio mabaya mwaka 2018 na 2019.

Waendesha mashtaka wa Rwanda walikuwa wametaka apewe kifungo cha maisha na walikuwa wameonyesha kutofurahishwa na uamuzi wa kutoa adhabu nyepesi kuliko walivyotaka.

Rusesabagina alikuwa amejiondoa kwenye kesi hiyo, ambayo vikundi vya haki, wafuasi na familia yake waliitaja kama kandamizi.

Yeye wala mawakili wake hawakuwa kortini kwa uamuzi huo, ambapo washtakiwa wenzake walihukumiwa kwa kati ya miaka mitatu hadi 20.

Siku ya Jumatano, binti ya Rusesabagina Carine Kanimba alisema hatua ya upande wa mashtaka kukata rufaa kwa hukumu hiyo ilionyesha kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa.

Korti ya rufaa inapaswa kuamua baadaye tarehe ambayo itaanza kusikiliza rufaa hiyo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...