Search This Blog

Saturday, October 23, 2021

Urusi na china zimefanya doria ya pamoja katika bahari ya Pasifik


Meli za kivita za Urusi na China zimefanya doria ya kwanza ya pamoja ya kijeshi katika eneo la Magharibi la bahari ya Pasifiki. Ikithibitisha habari hizo wizara ya ulinzi ya Urusi imesema zoezi hilo lilianza Oktoba 17 hadi 23.
 
Serikali za Moscow na Beijing, ambazo zilifanya mazoezi ya pamoja katika eneo la bahari ya Japan mapema Oktoba, zimezidi kuimarisha uhusiano wa kijeshi na kidiplomasia katika miaka ya hivi karibuni, katika kipindi ambacho pia uhusiano wao na mataifa ya Magharibi ukiwa umevurugika.
 
Operesheni hiyo ya kijeshi imekuwa ikifuatiliwa na Japan ambayo mapema wiki hii ilisema kundi la meli 10 kutoka China na Urusi zimeonekana zikipita katika ujia wa bahari wa Tsugaru, ambao unaigawa Japan Bara na kisiwa chake cha kaskazini cha Hokkaido.
 
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema doria hiyo ina lengo la kudumisha amani na utulivu katika eneo la Asia-Pasifik na uangalizi wa masuala ya shughuli za kiuchumi katika eneo la bahari baina ya mataifa hayo mawili.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...