Naibu Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia, Matteo Salvini leo hii anatarajiwa kupandishwa kizimbani huko katika mji mkuu wa mkoa wa Sicily, Palermo, kutokana na kuhusika kwake na kuizuia meli ya kunusuru wahamiaji kutia nanga katika bandari ya taifa hilo.
Upande wa mashataka unamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kutumia madaraka yake vibaya kuzuia meli ya uokozi iinayoitwa OpenArms, ambayo ilikuwa na wahamiaji 160.
Tukio hilo lililotokea Agosti 2019 wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani.Salvini amabae anatazamwa kama mtu mwenye sera zinazopinga wahamiaji, kwa mara kadhaa alirejea kusisitiza kuwa uamuzi wake huo ulikuwa na lengo la kulinda maslahi ya Italia na serikali.
Kesi hiyo ilianza rasmi mnamo Septemba 15, na kuahirishwa katika kipindi kifupi na sasa inatarajiwa tena kusikilizwa leo.
No comments:
Post a Comment