Search This Blog

Friday, October 1, 2021

UN yashangazwa na Ethiopia kwa kuwafukuza maafisa wake wakuu


Umoja wa Mataifa (UN) imeelezea kushtushwa kwake na hatua ya Ethiopia kuwafukuza nchini humo maafisa wake wakuu.

Hii ni baada ya Ethiopia kuwapa maafisa saba wakuu wa Umoja huo muda wa saa 72 kuondoka nchini humo "kwa kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi", kupitia ujumbe wa Tweeter kutoka kwa wizara ya mambo ya nje.

Katibu Mkuu António Guterres amesema UN inashirikiana na serikali "kwa matarajio kwamba "wafanyikazi walioathiriwa n ahatua hiyo wanaweza "kuendelea na kazi yao muhimu".

Maafisa hao ni pamoja na wakuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, Adele Khodr, na kaimu mkuu wa ofisi ya masuala ya binadamu Grant Leaity,UNOCHA.

Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulieelezea wasiwasi wake kufuatia ya hatua ya kuwekwa kwa vizuizi vya misaada kufika eneo la Tigray linalokumbwa na mzozo.

Inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tano kaskazini wanahitaji msaada wa kibinadamu.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...