Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekanusha kufanya mazungumzo juu ya haki ya wapenzi wa jinsia moja katika alipohudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
Uhusiano wa jinsia moja umepigwa marufuku nchini Zambia, ambako sheria za enzi za ukoloni wa Uingereza juu ya mapenzi ya jinsia moja bado zinatumika.
Rais Hichilema alitoa tamko hilo siku ya Alhamisi wakati wa hotuba yake kwa taifa iliyorushwa moja kwa moja kutoka mji mkuu, Lusaka baada ya kuombwa aweke wazi aliyoangazia katika ziara yake.
No comments:
Post a Comment