Na Maridhia Ngemela,Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa nguvu zote kutokana na jitihada zake za kuleta maendeleo.
Dkt Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kutoa mrejesho wa vikao vya bunge la bajeti na kushukuru wananchi kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu ulioisha mwaka jana eneo la Kisiwa Cha Bezi Kata ya Kayenze ambapo amesema kuwa zaidi ya Milioni 385 zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ndani ya kata ya Kayenze, Milioni 250 ya ujenzi wa kituo Cha afya Kayenze, Milioni 60 ya ukamilishaji wa maabara mbili za shule ya sekondari Kayenze, Milioni 50 ya Zahanati katika Kisiwa Cha Bezi, Milioni 10 ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Bezi na Milioni 15 ya shule ya msingi Kayenze
"Kama Kuna watu wananufaika na jitihada za Rais Mhe Samia basi wana Ilemela mnaongoza kwa matunda hayo maana kila niliomba napewa kikubwa na sisi kama wananchi tuzitumie vizuri miundombinu ambayo Serikali yetu inatutengenezea na tujitoe pia pale tunapoweza ili kuendeleza maendeleo ambayo tunatamani kuwa nayo ndani ya Jimbo letu hili alisema Mbunge.
Aidha Mhe Dkt Mabula akawataka wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 sambamba na kuwasisitiza kujitokeza kwaajili ya chanjo Ili wasiweze kupata athari zaidi pindi wanapopata maambukizi ya ugonjwa huo kwani athari za ugonjwa kwa mtu aliyechanjwa ni tofauti na zile za mtu ambae hakupata chanjo.
Kwa upande wake Mhandisi Mndeme kutoka wakala wa Barabara za mijini na vijijini TARULA wilaya ya Ilemela mbali na kupongeza jitihada zilizofanywa na Mbunge huyo katika kuhakikisha bajeti inaongezeka mpaka kufikia bilioni tatu kitu ambacho hakijawahi kutokea hivyo kuwaasa kuendelea kushirikiana Ili miradi yote iliyokusudiwa iweze kukamilika
Nae Afisa Ardhi mteule wa Manispaa ya Ilemela Bi Biligita Msandya amewataka wananchi wa kata hiyo wanaodai fidia za ardhi kuwa wavumilivu kwani Serikali inaitambua changamoto hiyo na watakuwa wakilipa awamu Kwa awamu mpaka madeni yote ya fidia yatakapokwisha.
Moja ya mwananchi aliyehudhuria mkutano huo uliofanyika Kayenze senta Bi Joyce Desdudit amefafanua kuwa anaridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan sanjari na kuwaomba kuungana pamoja kuhakikisha nchi inasonga mbele.
Search This Blog
Saturday, October 9, 2021
Tumuunge Rais wetu mkono kazi anayoifanya tunaiyona ndugu zangu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment