Search This Blog

Saturday, October 9, 2021

Ndugai apangua kamati za Bunge, Polepole ahamishwa


Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amehamishiwa kutoka Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenda kamati ya Sheria ndogo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 na Spika wa Bunge, Job Ndugai imeeleza kuwa mabadiliko hayo madogo ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge yamefanyika kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 135 (3) – (5) ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la Juni 2020.

Mabadiliko mengine ambayo Spika ameyafanya ni kumhamisha Godwin Kunambi kutoka kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenda Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Pamoja na hao Spika amewateua baadhi ya wabunge katika kamati kadhaa ambapo  Asia Halamga na Agnes Marwa wamepelekwa Kamati ya Masuala ya Ukimwi.

Pia, amemteua Dk Faustine Ndugulile kuwa mjumbe wa kamati ya sheria ndogo na kamati ya masuala ya Ukimwi.

Dk Medard Kalemani na Dk Leonard Chamuriho wameteuliwa kuwa wajumbe wa kamati ya sheria ndogo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...