Search This Blog

Tuesday, October 5, 2021

Tiba ya mpya ya kwanza ya seli mundu katika miaka 20


Tiba ya kwanza ya seli mundu katika kipindi cha miaka 20 itasaidia kuwazuwia maelfu ya watu kutoenda hospitalini kwa miaka mitatu ijayo, imesema Wizara ya huduma za afya nchini uingereza.

Ugonjwa wa seli mundo hautibiwi na unawaathiri mamilioni ya watu duniani.

Nchini Uingereza taasisi ya kitaifa ya huduma za afya imesema tiba hii itasaidia kupunguza kutokuwepo kwa usawa wa huduma za afya kwa watu weusi, ambao ndio wanaoathiriwa zaidi na mara nyingi wanakuwa na afya duni kutokana na maradhi hayo.

Dawa hiyo imeitwa "tiba ya uvumbuzi".

Maumivu

Dawa hiyo, crizanlizumab, ambayo imetengenezwa na Novartis, huchomwa kwenye mshipa na inaweza kutumiwa pamoja na dawa za kawaida pamoja na uongezewaji wa damu.

Sarah-Jane mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akiugua seli mundu, jambo ambalo lilimfanya kukata tamaa ya njozi yake ya kuwa mwalimu wa chekechea kwasababu kazi hii ingemuweka katika hatari ya maambukizi.

"Sasa, nimepata sababu ya uhakika na ningependa kueneza uelewa kuhusu malazi ya seli mundu," anasema.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...