Search This Blog

Sunday, October 3, 2021

Tetesi za soka Ulaya leo 03.10.2021

Manchester United wanataka mpaka kufikia Christmas uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wa kiungo mfaransa Paul Pogba uwe umefikiwa. (Sun)


Manchester City wanaamini wako kwenye nafasi nzuri kuliko wapinzani wao Liverpool, Manchester United, Chelsea na Bayern Munich kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Benfica raia wa Uruguay Darwin Nunez, 22. (Star)

Kiungo wa Leeds na timu ya taifa ya England Kalvin Phillips ana nia ya kusaini mkataba mpya ulioboreshwa ili kuendelea kusalia Elland Road.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 amesalia na miaka miwili katika mkataba wake wa sasa. (Athletic - subscription required)


Mshambuliaji wa Manchester United raia wa Uruguay Edinson Cavani, 34, anaweza kujiunga na Real Madrid mwezi January, baada ya kutokua chaguo la kwanza Old Trafford kufuatia ujio wa Cristiano Ronaldo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Bayern Munich wanakaribia kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mshambuliaji wake mjerumani Serge Gnabry, 26. (Fabrizio Romano on Twitter)

Paris St-Germain wameripotiwa kutaka kujaribu kurusha ndoano kumsajili mshambuliaji raia wa Norway Erling Braut Haaland, 21 kutoka Borussia Dortmund msimu ujao. (Mirror)

Kiungo wa Cagliari Nahitan Nandez, 25, anatarajia kuikacha klabu hiyo kwa mujibu wa wakala wake. Nyota huyo wa Uruguay amekuwa akiwaniwa na vilabu vya Tottenham, Leedpamoja na Napoli. (Calcio Napoli 24 - in Italian)

Steve Bruce ataendelea kuwa meneja wa Newcastle wakati huu ambapo kipaumbele kikubwa cha mmiliki wa klabu Mike Ashley kusaka mnunuzi wa kuinunua klabu. (Sun)

Mshambuliaji mfaransa Karim Benzema, 33, hana shaka yoyote kwamba mfaransa mwenzie, mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, siku moja atajiunga na Real Madrid. (L'Equipe via Sun)

Vilabu vya West Ham, Everton na Arsenal vinamtaka mshambuliaji wa Real Betis Nabil Fekir lakini Betis nao wanataka kuendelea kupata huduma ya mfaransa huyo mwenye miaka 28. (Fichajes - in Spanish)

Real Madrid wanafikiria kumsajili kiungo mbelgiji wa Leicester Youri Tielemans, 24, lakini ujio wake utaonyesha ishara ya kuondoka kwa kiungo wa kibrazil Casemiro, 29, kuelekea Paris St-Germain. (El Nacional)

Katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani Barcelona watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26 ili kucheza La Liga. (OnzeTV on Twitter)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...