Search This Blog

Sunday, October 3, 2021

Ajali yaua watu wawili Tarime

 Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana eneo la Gamasara wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/ Rorya,  William Mkonda amesema ajali hiyo imetokea leo Oktoba 3, 2021  saa 3.15 asubuhi.

Amesema ajali hiyo imehusisha basi la Kampuni ya Zakaria na  gari aina ya Nissan Safari.

Kamanda Mkonda amesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani hali iloyosababishwa na dereva wa basi.

"Dereva aliamua kupita magari kadhaa barabarani bila kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ndipo akakutana uso kwa uso na gari dogo, ajali hii imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali," amesema Kamanda Mkonda.

Hata hivyo, amesema kuwa majina ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo bado hayajapatikana na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...