Search This Blog

Saturday, October 23, 2021

Taulo za kike 2500 zatolewa kwa shule za sekondari Rufiji

Kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kitaifa leo
Oktoba 23, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gaudentia Kabaka ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Rufiji na kukabidhi mashuka 100 sambamba na kukabidhi taulo za kike 2500 kwa Shule ya Sekondari Utete na Ikwiriri.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kabaka amesema UWT ni jumuiya ambayo imekua ikiunga mkono jitihada za Serikali katika sekta mbalimbali hivyo katika kuadhimisha kilele cha wiki yao wameona ni vema wazifikie jamii moja kwa moja.

Kabaka amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha sekta ya elimu na kuwainua wanawake nchini.

Amewaeleza wanafunzi hao umuhimu wa elimu kwa maisha yao ya baadaye.

"UWT Taifa tumefika hapa kuzungumza na nyinyi mabinti wasomi, tumewaletea taulo hizi zipatazo 2500 kwa shule hizi mbili za Ikwiriri na Utete ambazo naamini zitawasaidia kutatua changamoto zenu za kila mwezi za kimaumbile ambazo kwa namna moja ama nyingine huwazuia kuhudhuria masomo yenu.

"Ziepukeni Ndoa za utotoni lakini pia msikubali kupata mimba ili muendelee na elimu na kuweza kufikia malengo yenu, tunaamini ndani ya kundi hili kuna akina Rais Samia wengi, kuna Mwenyekiti wa UWT na mawaziri wengi sana, someni Taifa linawategemea," amesisitiza Kabaka.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...