
Jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika, SADC, imekubali kuongeza zaidi uwepo wa vikosi vya kikanda vinavyopambana na waasi kaskazini mwa Msumbiji.
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amethibitisha kurefushwa zaidi kwa muda wa vikosi hivyo Jumanne jioni katika mwisho wa kikao kisicho cha kawaida.
Awamu ya kwanza ya upelekaji wa vikosi hivyo ilipangwa kukamilika tarehe 15 Oktobar.
Kikao hicho kiliitishwa kutathmini utendaji wa vikosi vya kikanda.
Rais Nyusi alisema kuwa Msumbiji iliridhishwa na tathmini iliyofanywa sasa na kwamba hali imeimarika kwa kiasi kikubwa katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kikao hicho kilitoa heshima kwa wanajeshi waliofariki wakiwa kazini nchini Msumbiji. Watatu hao walikuwa ni kutoka mataifa ya Tanzania na Botswana.
No comments:
Post a Comment