Search This Blog

Friday, October 15, 2021

Rais wa Sudan kusini amfukuza bosi wa kampuni ya mafuta


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfukuza bosi wa kampuni ya mafuta bwana Bol Ring Mourwel.

Hakuna taarifa iliyotangazwa kueleza sababu ya kufukuzwa kwake na rais, televisheni ya nchi ilisema Alhamisi usiku.

Bosi mpya wa Nile Petroleum Corporation (Nilepet) bado hajachaguliwa.

Aidha bado haijawekwa wazi kama kufukuzwa kwake kuna uhusiano na madai kuhusu bwana Bol kuhamisha fedha za kiasi cha $250m (£182m) katika benki yake binafsi iliyoko Dubai na Khartoum. Ingawa alikanusha madai hayo.

Bwana Bol alichaguliwa mwaka jana ,na kuchukua nafasi ya Chol Deng Thon.

Alichaguliwa kusimamia Nilepet kukiwa na mipango ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi katika taifa hilo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...