Search This Blog

Friday, October 15, 2021

Poland yapitisha sheria kuwazuia wahamiaji mpakani


Bunge la Poland limepitisha marekebisho ya sheria yanayoruhusu wahamiaji kuzuiwa mpakani na vilevile maombi ya hifadhi kutoka kwa wahamiaji walioingia nchini humo kinyume cha sheria yapuuzwe.
 
 Wabunge pia waliridhia mpango wa serikali kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji wanaovuka kutoka Belarus. 
 
Haya yanajiri wakati katika miezi ya hivi karibuni, maelfu ya wahamiaji wengi kutoka Mashariki ya Kati wamekuwa wakijaribu kutoka Belarus kuingia Poland au Latvia na Lithuania.
 
 Mashirika ya kutetea haki, tayari yameishutumu Poland kwa kuwazuia wahamiaji mpakani na kuwalazimisha kurudi Belarus.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...