Search This Blog

Wednesday, October 6, 2021

Princess Haya: Mtawala wa Dubai aliagiza kudukuliwa kwa simu ya mke wake wa zamani


Mahakama kuu nchini Uingereza imegundua kwamba mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed Al Maktoum, aliingilia mfumo wa haki ya Uingereza kwa kuagiza kudukuliwa kwa simu ya mkewe wa zamani, Princess Haya wa Jordan.

Simu za mawakili wake, Baroness Fiona Shackleton QC na Nick Manners, pia zililengwa wakati wa kesi yao ya talaka, kulingana na korti.

Princess Haya alisema ugunduzi huo ulimfanya ahisi "kuwindwa ".

Sheikh Mohammed alikanusha ufahamu wowote wa udukuzi huo.

Alisema matokeo ya korti yalitokana na ushahidi ambao haukujulishwa kwake, na kwamba "Yalifanywa kwa njia ambayo haikuwa ya haki".

Ugunduzi huo ni pigo kwa kiongozi huyo juu ya jinsi anavyowatendea wanawake katika familia yake.

Hukumu za Mahakama Kuu, ambazo zilichapishwa Jumatano alasiri, zilitaja udukuzi huo kama "ukiukaji wa sheria za (Uingereza) za uhalifu wa ndani", "kwa kukiuka sheria ya msingi ya kawaida na haki za ECHR", "kuingiliwa na mchakato wa korti hii na upatikanaji wa haki kwa mama’ "na" matumizi mabaya ya madaraka "na mkuu wa serikali.

Rais wa Idara ya Familia ya Mahakama Kuu aligundua kuwa "simu za mama (Princess Haya), mawakili wake wawili, msaidizi wake wa kibinafsi na wafanyikazi wake wawili wa usalama zilikuwa zimeingiliwa au jaribio kutekelezwa kutumia Programu inayoitwa Pegasus ya kampuni ya Israeli, NSO. "

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...