Search This Blog
Friday, October 15, 2021
Naibu waziri akerwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Hoteli
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amekagua ujenzi wa Hoteli ya Kitalii ya nyota tatu katika eneo la Lubambangwe Burigi wilayani Chato kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hoteli hiyo inayotarajiwa kutumika kwa ajili ya watalii watakaotembea maeneo ya vivutio vya Utalii Wilayani humo.
Amefanya ziara hiyo ya kushtukiza jana kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa hoteli hiyo.
Masanja amemuelekeza Mwakilishi wa Mradi huo kutoka TANAPA, Jeremiah Machibya kumsimamishia mkataba mkandarasi huyo kama ameshindwa kumaliza kazi kwa muda unaotakiwa.
"Kama mkandarasi kazi imemshinda tengueni mkataba muweke anayeweza kuimaliza kazi hii kwa wakati," Masanja amesisitiza.
Mradi huo wenye gharama ya shilingi bilioni 11 unaosimamiwa na TANAPA ulianza Aprili 2020 na ulitarajiwa kukamilika Aprili, 2021 lakini mkandarasi ameongezewa muda hadi mwezi Machi, 2022.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment