Search This Blog

Sunday, October 10, 2021

Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Wafikia Asilimia 82


AIBU Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Rusumo umefikia asilimia 82 ya utekelezaji na kwamba mkandarasi ameshalipwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Disemba mwaka huu.


“Tumejadili kwa pamoja maendeleo ya ujenzi wa mradi huu wa Rusumo, tumeridhishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea, pia fedha za kuhakikisha mradi huu unakamilika kama ulivyopangwa zipo tayari,” alisema wakati wa Mkutano wa 13 wa Mawaziri uliomalizika kwa ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo uliopo Ngara mkoani Kagera.


Mradi huo ulipangwa kugharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 75 hata hivyo mkandarasi amelipwa Dola milioni 89 sawa na asilimia 114 ya gharama ya awali. Mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 80, ambazo zitagawanywa katika nchi Burundi, Rwanda na Tanzania ambapo kila nchi itapata Megawati 26.6 kwa ajili ya matumizi ya nchi yake.


Mwenyekiti wa mawaziri wa nishati ambaye ni Waziri wa Nishati na Miundombinu kutoka Rwanda,  Claver Gatete, aliwaongoza mawaziri; Naibu Waziri Byabato kutoka Tanzania na Waziri wa Nishati wa Burundi, Ibrahim Uwizeye  kutembelea mradi huo ili kuona maendeleo ya mradi ulikofikia.


Mara Baada ya ukaguzi wa Mradi mawaziri hao pamoja na Wajumbe wa bodi walikutana  katika kikao Cha majadiliano kwa ajili ya kujadili maendeleo ya mradi na changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza wakati mradi ukiendelea  na Mara Baada ya kikao mwenyekiti wa mawaziri hao kutoka Rwanda Claver Gatete alisema wanafurahishwa na Kasi ya mradi unavyoendelea.


Aidha alitaja mabadiliko mbalimbali ambayo yamejitokeza katika mradi huo kuwa  ni awali nchi zilikubariana   kuzalisha na kusambaza umeme katika nchi zao lakini mabadiliko yaliyotokea ni kuhakikisha  vituo vya kupokea umeme  vitasambaza umeme kutoka katika miradi mingine  inayoratajia kukamilika hivi karibuni ili kufanya umeme kuendelea kuwepo  hata Kama mradi mmoja utapata changamoto yeyote.


"Tumejipanga vizuri kwamba Tanzania tunatakiwa kusambaza umeme  katika nchi Jirani hii itakuwa Biashara nzuri kwetu hivyo kupitia mradi huu  tuliona Ni vyema  vituo vya kupokea umeme vilivyojengwa viwe na uwezo Wa kupokea umeme wetu kutoka katika miradi mingine ambayo itakamilika hivi karibuni   hivyo Tanzania itaendelea kufanya Biashara kwa kuuza umeme wake katika nchi Nyingine, na vituo vyote vitakuwa na uwezo Wa kupokea umeme kutoka katika vyanzo vyote vya umeme"alisema Byabato.


Hata hivyo mawaziri wote wa nchi tatu  walihitimisha kwa kuitaka bodi kusimamia majukumu yake  vizuri na kuwasimamia wakandarasi  ili mradi huo ukamilike kwa haraka kwa sababu wananchi wanachohitaji ni umeme.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...