Miungano miwili ya upinzani imekishinda chupuchupu chama cha Waziri Mkuu Andrej Babis ANOP kwenye uchaguzi wa jana wa bunge wa Jamhuri ya Czech.
Miungano hiyo ya vyama vya kisiasa ya Pirates na Mayors imesema inataka kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto. Ushindi huo wa kustaajabisha unaweza kuwa ndiyo mwisho wa uongozi wa bilionea Babis.
Muungano wa vyama vitatu vya kihafidina wa Together umepata asilimia 27.8 ya kura, wakati kundi lengine la upinzani la vyama vya Pirates na Mayors limepata asilimia 15.6 ya kura. Miungano hiyo miwili kwa pamoja imepata viti 108 katika bunge lenye viti 200.
Kiongozi wa muungano wa Pirates na Mayors, Ivan Bartos, amesema wataanza mazungumzo ya kuunda serikali ijayo. Chama tawala cha ANO, kinachoongozwa na bilionea huyo maarufu Babis, kilimaliza katika nafasi ya pili, kwa kupata asilimia 27.1 ya kura.
No comments:
Post a Comment